Overview
Artist: The song is performed by a Taarab artist, known for their poetic lyrics and rich melodies typical of the Taarab genre, which blends Swahili, Arabic, and African musical elements.
Album: “Kwa Raha Zangu Taarab” showcases the artist’s ability to convey deep emotional and spiritual mes...
MLANGO WA MUNGU UWAZI
Mja hufiki popote, ni bure chako kiburi
Dunia ni yetu sote, tajiri na mafakiri
Mja hufiki popote, ni bure chako kiburi
Dunia ni yetu sote, tajiri na mafakiri
Jua wabaya si wote, wapo watonistiri
Jua wabaya si wote, wapo watonistiri
Riziki hutoi wewe, mja usitakabari
Riziki hutoi wewe, mja usitakabari
Ooohhh lalaalala
Ukinisusia wewe, sishituki moyo wangu
Sishituki moyo wangu
Nitapata mwenginewe, atojali shida zangu
Atojali shida zangu
Ukinisusia wewe, sishituki moyo wangu
Sishituki moyo wangu
Nitapata mwenginewe, atojali shida zangu
Atojali shida zangu
Hasama mimi na wewe, si kusudio langu
Ukinibagua wewe, hanitupi Mola wangu
Ooh hasama mimi na wewe, si kusudio langu
Ukinibagua wewe, hanitupi Mola wangu
Kama wewe ni mbaya, nao wema wapo tele
Kama wewe ni mbaya, nao wema wapo tele
Chorus
Jua mlango wa Mungu, uwazi kaufungua
Kama riziki ni yangu, huwezi kuiondoa
Jua mlango wa Mungu, uwazi kaufungua
Kama riziki ni yangu, huwezi kuiondoa
Ufanyaje mlimwengu, usiyekuwa na haya
Utamaliza mizungu, la Mola hutopangua
Ufanyaje mlimwengu, usiyekuwa na haya
Utamaliza mizungu, la Mola hutopangua
Verse 2
Mhh
Madhali ni hai,Sina wasiwasi
Kwa riziki yangu,Kwa Mola Ilahi
Najua sikosi,Nna langu fungu
Madhali ni hai,Sina wasiwasi
Kwa riziki yangu,Kwa Mola Ilahi
Najua sikosi,Nna langu fungu
Taji hunivui,Hili lishapasi
Sijipe uchungu.Choyo hakifai
Na chuki binafsi,Ewe mlimwengu
Taji hunivui,Hili lishapasi
Sijipe uchungu.Choyo hakifai
Na chuki binafsi,Ewe mlimwengu
Ukiufunga wa kwako mlango
Juwa wa Mungu uwazi.Ukiufunga wa kwako mlango
Juwa wa Mungu uwazi
Verse3
Umekaza uzi,Kunichonganisha,Kwa mashoga zangu
Nalijua wazi,Linokukondesha,Ni bahati yangu
Umekaza uzi,Kunichonganisha,Kwa mashoga zangu
Nalijua wazi,Linokukondesha,Ni bahati yangu
Unajipa kazi,Hutoiondosha
Kudura ya Mungu.Hayo huyawezi
Wajihangaisha,Yawache majungu
Unajipa kazi,Hutoiondosha
Kudura ya Mungu. Hayo huyawezi
Wajihangaisha,Yawache majungu
Unajipa kazi,Hutoiondosha
Kudura ya Mungu. oohhh Hayo huyawezi
Wajihangaisha,Yawache majungu
Sote wa kukadiriwa na Mungu,Hatujitoshi kwa kitu
Sote wa kukadiriwa na Mungu,Hatujitoshi kwa kitu
Atowaye ni Kahari, kwa matamu machungu,kwa matamu machungu
Usijipe ujabari, kuvaa joho la Mungu,kuvaa joho la Mungu
Atowaye ni Kahari, kwa matamu machungu,kwa matamu machungu
Usijipe ujabari, kuvaa joho la Mungu,kuvaa joho la Mungu
Haufai ujeuri, ewe kiumbe mwenzangu
Tuendako ni shubiri, mwanandani letu fungu
Oohh Haufai ujeuri, ewe kiumbe mwenzangu
Tuendako ni shubiri, mwanandani letu fungu
Joho la MwenyenziMungu, mja likufae wapi
Joho la MwenyenziMungu, mja likufae wapi
Chorus
Jua mlango wa Mungu, uwazi kaufungua
Kama riziki ni yangu, huwezi kuiondoa
Jua mlango wa Mungu, uwazi kaufungua
Kama riziki ni yangu, huwezi kuiondoa
Ufanyaje mlimwengu, usiyekuwa na haya
Utamaliza mizungu, la Mola hutopangua
Ufanyaje mlimwengu, usiyekuwa na haya
Utamaliza mizungu, la Mola hutopangua
Jeuri ya nini wewe,hukujiumba umeumbwa
Umezidi ni wewe,kiburi chako ni buree
Mlango wa mungu uko wazi,Ridhiki napata mimi
Ninarutubiwa mimi,Mungu amenistiri
Mlango Wa Mungu Uwazi was written by SABAH SALUM.
Mlango Wa Mungu Uwazi was produced by East African melody.