[Intro: Andre K]
Subiri mkeka … subiri mkeka
Its Andre K
[Verse 1: Andre K]
Hapa nshaweka nadhiri, mpaka nipige hizo pesa
Nina mipango kamili, ya kuwa Tajiri ka ndesa
Kwanza naamka saa 2, usafi wa mwili ka Jombira
Kisha nacheki na shiling ntalipa bili, supu chapati kwa Bob Chaa
Napitia vocha kwa mnama, nipate dakika bando
Narudi ghetto nainama, vipi uhakika wa dabo
Mami anasema, hali mbovu, namjibu mamii,usiwe na hofu
Mkeka wa juzi alichana juve, acha leo Man afungwe
Naona milioni kwenye odds nying, naanza kuchambua siweki pozi dingi
Demu wangu anataka nae kwenda saloon
Hataki kwenda kesho namuweka mbavuni
Mhindi akilia mamii utacheka
Ngoja hiyo kesho subiri mkeka
[Hook: Andre K]
Subiri subiri, subiri mkeka
Subiri subiri, subiri mkeka
Mhindi akilia mamii utacheka
Ngoja hiyo kesho subiri mkeka
Subiri subiri, subiri mkeka
[Verse 2: Slimsal]
Nikibashiri kuwa nani atashinda, nimejitabiri bingwa
Uhakika wa utajiri ninja, kesho nabadili jina
Tajiri mimi maskini Bakhera, kama huamini subiri mkeka
Huo huo muda wa pepa, hiyo pesa! Mhindi akilia mamii utacheka
Mh! Unasononeka ukiona magari wеnzako wanaendesha
Punguza presha na kama hauwеzi kulala kesha
Lakini kesho, kitaeleweka. Yale mateso, yatatoweka
Lala na gubu uamke na vogue, ulilipa kodi utakusanya kodi
Maana, naona milioni kwenye odds kibao, mabosi zangu kesho mi ndo bosi wao
Usifikiri unavyoniona nipo busy tu na simu labda naangalia mademu wa kwenye mitandao
Mkeka bila game nyingi hauoni, ndo utajiri unapobishaga hodi
So mami usifikiri nacheza, ngoja hiyo kesho Aika, subiri
[Hook: Andre K]
Subiri mkeka Subiri subiri
Mhindi akilia mamii utacheka
Subiri mkeka
Ngoja hiyo kesho subiri mkeka
Subiri subiri, subiri mkeka
[Outro: Slimsal]
Yoh Andre k, I miss you bro
I miss you bro… ah man, asante kwa kuniachia vocal zako
Najua ulikuwa unataka tufanye mengi sana but, mipango ya mungu
RIP my brother, I love you
Washkaji zako DDC nikiwaangalia naona pain
Mungu ndiye ambaye anajua siri ya kifo ni nini
Unanikumbusha Godzilla, kuondoka kwako
Sababu mara ya kwanza nakutana na Godzilla nilikuwa na wewe Andre K
So hizo ni memory ambazo zinaniumiza sana
Mungu akulaze mahali pema Rafiki yangu
Na nataka nikufahamishe baada ya Godzilla, wewe
Nimepoteza pia baba yangu mzazi
So mwambia baba huko aliko, huku kuna mengi sana yanaendelea
I feel like am Blind
SUBIRI MKEKA was written by SLIMSAL.
SUBIRI MKEKA was produced by SLIMSAL.
SLIMSAL released SUBIRI MKEKA on Fri Feb 26 2021.