[Verse 1]
Kwa goti aliingia
Nakutaka nimsamehe
Kumbe ananichora
Mapenzi yalinijia
Kwenye moyo shurba tele
Ya-radhi akanijia
Kidudu mtu shetani akayavuruga
Akaingia mashakani tukashindwana
Kidudu mtu shetani akayavuruga
Akaingia mashakani tukakwazana
[Pre Chorus]
Nimeamini kwenye moyo huwezi penda mara mbili
Penzi ukalitia kasoro maskini mimi
Moyo wangu sio godoro, uwe juu me niwe chini
Si kisoda kwa kokoro, nimeshindwa mimi yeah
[Chorus]
Aaah haya nimeridhia (sawa)
Siwezi ng'ang'ania (sawa)
Aah haya nimeridhia (sawa)
Nimeshindwa mimi
Aaah haya nimeridhia (sawa)
Siwezi ng'ang'ania (sawa)
Aah haya nimeridhia (sawa)
Nimeshindwa mimi
[Verse 2]
Kweli sio siri, ilizingwa mapema
Tamu yako ya asili, ila ndani yachoma
Kheri kuwa dhahiri, maumivu kusema
Mlaghai kwa hili, nafsi yangu imenena
Nashukuru kwa kidogo, ulichonipa nimepokea
Nitabaki kwa mikogo, huyo mwengine kumngojea
[Pre Chorus]
Nimeamini kwenye moyo huwezi penda mara mbili
Penzi ukalitia kasoro maskini mimi
Moyo wangu sio godoro, uwe juu me niwe chini
Si kisoda kwa kokoro, nimeshindwa mimi yeah
[Chorus]
Aaah haya nimeridhia (sawa)
Siwezi ng'ang'ania (sawa)
Aah haya nimeridhia (sawa)
Nimeshindwa mimi
Aaah haya nimeridhia (sawa)
Siwezi ng'ang'ania (sawa)
Aah haya nimeridhia (sawa)
Nimeridhia was produced by Ringtone.
Maua-sama released Nimeridhia on Fri May 20 2022.